Man United wampa mkulima jukumu la kutunza uwanja!
Eric Buyanza
December 6, 2023
Share :
Klabu ya Manchester United imemkabidhi jukumu maalum mkulima maarufu nchini Uingereza, Bwana Kaleb Cooper.
Bwana Cooper amepewa heshima na jukumu la kutunza nyasi za uwanja wa Old Trafford kwa ajili ya mchezo dhidi ya Chelsea utakaochezwa Jumatano usiku.
Cooper ni mmiliki wa shamba maarufu la Clarkson's Farm na shabiki lialia wa Man United.