Man United wana bajeti ya Pauni milioni 45 kwa ajili ya beki wa kati
Eric Buyanza
June 8, 2024
Share :
Mashetani wekundu (Man United) wameandaa bajeti ya pauni milioni 45 kwa ajili ya kusajili beki wa kati atakayeimarisha safu yao ya ulinzi msimu ujao, huku tayari wakiwa na majina ya wachezaji watatu muhimu kwenye daftari lao.
Chaguo lao nambari moja ni mfaransa Jean-Clair Todibo mwenye umri wa miaka 24 anayechezea klabu ya Nice, na endapo wakishindwa kupata saini ya mfaransa huyo basi machaguo mengine ni Gonçalo Inacio wa klabu ya Sporting CP ya Ureno au Leny Yoro mwenye umri wa miaka 18 anayekipiga na Lille ya Ufaransa ambaye amekuwa akisakwa na vilabu vingi vikubwa barani Ulaya ikiwemo Real Madrid.