pmbet

Man United yauza nyasi za zamani za Old Trafford, kipande kwa 437,000 /=

Eric Buyanza

September 24, 2026
Share :

Klabu ya soka ya Manchester United imeingia kwenye vichwa vya habari duniani kote, safari hii si kwa matokeo ya uwanjani, bali kwa mkakati wa kipekee wa kibiashara baada ya kuanza kuuza vipande vya nyasi halisi za uwanja wao wa Old Trafford kwa mashabiki, ambapo kila kipande kimoja kinauzwa kwa Pauni 125 (sawa na Shilingi za Kitanzania 437,000).

 

Bidhaa hiyo inayofahamika kama "Old Trafford Turf Cubes," ina ukubwa wa sentimita 7 kwa 7. Nyasi hizo zilizong'olewa zimehifadhiwa kitaalamu ndani ya kitalu cha glasi ngumu ili zisinyauke, na zimewekwa kwenye sanduku maalum la zawadi linaloambatana na cheti cha uthibitisho na picha ya uwanja huo wa kihistoria.

 

Uamuzi wa kukata na kuuza "sehemu hii ya historia" umekuja baada ya United kuubomoa kabisa uwanja wa Old Trafford mwezi Juni kwa ajili ya matengenezo makubwa ya mfumo wa chini.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet