Man united ‘yavamia’ Gambia kumnasa winga Alieu Saine
Eric Buyanza
October 3, 2026
Share :
Inaripotiwa kuwa Manchester United ni miongoni mwa klabu kadhaa kubwa za Ulaya zinazomfuatilia Alieu Saine, winga kijana kutoka Gambia.
Saine alionyesha kiwango bora katika mashindano ya WAFU Kanda A ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U-17), na kuisaidia Gambia kutwaa taji hilo.
Ni wazi kuwa United inaendelea kusaka vipaji vichanga vyenye uwezo mkubwa kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Je, ungependa kuona United ikimsajili?






