pmbet

Man Utd na Arsenal wakandana Pre-Season Marekani

Sisti Herman

July 28, 2024
Share :

Timu mbili zenye upinzani mkubwa kwenye ligi kuu Uingereza Manchester United na Arsenal leo alfajiri wamecheza mchezo wa maandalizi ya msimu mpya (Pre Season) kwenye dimba la Sofi Stadium jijini Los Angeles nchini Marekani na kugawana ushindi ambapo kwenye dakika 90 za mchezo Arsenal wameshinda kwa mabao 2-1 baada ya hapo zikapigwa penati United akashinda penalti 5-3.

Kwenye mchezo huo Magoli ya Arsenal kwenye ushindi wa dakika 90 yalifungwa na washambuliaji wawili raia wa Barzil Gabriel Jesus dakika ya 26 na Gabriel Martinelli dakika ya 81 huku goli pekee la Manchester United likifungwa na mshambuliaji raia wa Denmark Rasmus Hojlund dakika ya 10.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet