Man Utd vs Liverpool, hapatoshi leo EPL
Sisti Herman
April 7, 2024
Share :
Mahasimu wa kihistoria wa ligi kuu Uingereza Manchester United na Liverpool watakutana leo kwenye mchezo wa raundi ya 31 wa ligi hiyo utakaochezwa leo saa 11:30 jioni kwenye dimba la Old Trafford Manchester.
Liverpool wanaingia kwenye mchezo huo wakihitaji alama tatu ili kurejea kileleni mwa msimamo kuiondoa Arsenal ambayo baada ya ushindi wa jana dhidi ya Brighton ilifikisha alama 71 baada ya kucheza michezo 31 huku Liverpool wakishuka hadi nafasi ya pili wakiwa na alama 70 huku wakihitaji mchezo mmoja kurudi kileleni.
Man Utd wanaoingia dimbani leo walihitaji ushindi ili kuendelea kupata matumaini ya kumaliza nafasi nne za juu ili kucheza UEFA Champions league msimu ujao kwani hadi sasa wapo nafasi ya 6 wakiwa na alama 45, alama 12 nyuma ya Aston Villa waliopo nafasi ya 4.
Je nani kuibuka mbabe leo?