Man Utd wakubali kumnunua Mbeumo kwa pauni milioni 71
Eric Buyanza
July 18, 2025
Share :
Manchester United wanakaribia kukamilisha usajili wa Bryan Mbeumo baada ya kuafikiana na Brentford kulipa dau lililoboreshwa la pauni milioni 71, vyanzo vimeiambia ESPN.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon anatarajiwa kuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Ruben Amorim kipindi hiki cha usajili.
Kuna matumaini kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anaweza kufanyiwa vipimo vya afya mapema wikiendi hii na kuwa sehemu ya kikosi kitakachosafiri kuelekea Marekani Jumanne kwa ajili ya kuanza kwa ziara ya mechi tatu za Amerika.
#TetesiZaSoka