Man Utd yageukia kwa kiungo punda wa PSG
Sisti Herman
June 25, 2024
Share :
Klabu ya Manchester United ligi kuu Uingereza inahusishwa kuhitaji saini ya kiungo kati wa klabu ya PSG ya Ufaransa na timu ya Taifa Uruguay, Manuel Ugarte.
Ugarte ambaye yupo kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Uruguay inayoshiriki michuanio ya kombe la mataifa ya America (Copa America) alionyesha kiwango bora kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Panama, Uruguay ikishinda 3-1.
Ugarte anatajwa kuchukua nafasi ya Casemiro anayetajwa kuhitajika na timu za Saudi Arabia.