Man Utd yamsajili mshambuliaji kutoka Uholanzi
Sisti Herman
July 14, 2024
Share :
Klabu ya Manchester United ya ligi kuu Uingereza imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kati wa timu ya Taifa Uingereza na klabu ya Bologna ya ligi kuu Italia Joshua Zirkzee.
Joshua amesaini na kutambulishwa leo mbele ya kocha mkuu wa klabu hiyo Mholanzi Erik Ten Hag na ataitumikia klabu hiyo hadi mwaka 2029 mkataba uliogharimu ada ya uhamiho kiasi cha Euro milioni 45.5 zitakazolipwa kwa awamu tatu, wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.