pmbet

Man Utd yasema Kwaheri kwa Raphael Varane!

Eric Buyanza

January 1, 2024
Share :

Manchester United wameamua kutoongeza mkataba wa Raphael Varane kwa miezi 12 zaidi.
 

Varane sasa atakuwa huru kufanya mazungumzo na vilabu vingine kuanzia Januari 1.
 

Lakini pia Man United bado iko tayari kuendelea na Varane kwa kusaini nae mkataba mpya lakini kwa sharti la kupunguzwa mshahara.
 

Beki huyo wa kati kutoka Ufaransa mwenye umri wa miaka 30 alijiunga na Mashetani Wekundu mwaka 2021 kwa mkataba wa pauni milioni 41 kutoka Real Madrid.
 

Usajili huo ulionekana kuwa wa dhahabu kutokana na Varane kutwaa mataji manne ya Ligi ya Mabingwa akiwa Uhispania, lakini mambo hayakwenda kama ilivyotarajiwa.
 

Varane amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka katika kipindi chote cha msimu huu, huku Al Nassr na Real Madrid zikitajwa kumtaka.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet