Manara atamani derby ingepigwa Dar na siyo Zenji.
Joyce Shedrack
February 19, 2026
Share :
Diwani wa Kariakoo na Msemaji wa zamani wa wababe wa Kariakoo Haji Sunday Manara ametoa maoni yake kuhusu mchezo wa Kariakoo derby kuchezwa Visiwani Zanzibar tarehe 1 march huku akiweka wazi kuwa ni bora ingechezwa Dr es Salaam.

“Nimeambiwa Yanga na Simba wanaenda kucheza Zanzibar,Yanga ndo mwenyeji nirudie kauli ya Motsepe sisemi Zanzibar haistahili kuandaa mechi kubwa,Lakini hii mechi Yanga alikuwa anahitaji mapato ‘gate collections’kwa sababu wao ndo mwenyeji lakini kuna mashabiki wanatoka Mikoani kuna watu wanatoka Nzega,Mbeya,Tukuyu kufuata derby tu”,
“Mimi kwa uzoefu wangu robo ya mashabiki wanaokuja kuangalia derby wanatoka Mikoani,hao unawatesa wakifika Dar watafute boti kwenda Zanzibar,Wakifika Zanzibar hakuna guest kuna hotel gharama unamfanya shabiki akose hamu ya kuangalia derby”,
“Yanga na Simba bado zinategemea hela za watu wawili Ghalib Said na Mo Dewji tuwapunguzie hawa wafadhili wetu mzigo wa kuziendesha hizi timu,tiketi ya ndege atoe tena Ghalib au Mo kwanini isifanyike hapa tukajikita kwenye promo?”
“Baadhi ya watu wa Yanga waanamini mechi yoyote ikichezwa Zanzibar Yanga anashinda kitu ambacho siyo sahihi watu wanaongea bila data mimi nimeshashuhudia Yanga akifungwa Zanzibar si mara moja na Simba na hata mechi tulizoshinda Yanga hatukushinda kwa Margin kubwa kama tulizoshinda Dar es Salaam” Amesema Manara.





