Manchester City kunasa saini ya Rayan Cherki.
Joyce Shedrack
June 6, 2025
Share :
Klabu ya Manchester City imeanza rasmi mazungumzo na klabu Lyon ya Ufaransa ili kunasa saini ya kiungo mshambuliaji Rayan Cherki raia wa Ufaransa ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chao msimu wa 2025/26.
/origin-imgresizer.tntsports.io/2025/04/10/image-09c128a8-dfa9-4f51-96ae-f97dcc771d68-85-2560-1440.jpeg)
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 amefunga mabao 8 na kutoa pasi 11 za magoli katika michezo 30 aliyocheza kwenye ligi kuu ya Ufaransa msimu uliopita.
Mchezaji huyo ambaye siku ya jana alionesha kiwango bora katika dakika 26 tu alizocheza kwenye Nusu Fainali ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya dhidi ya Hispania akifunga goli 1 na kutoa pasi 1 ya goli mkataba wake na klabu Lyon unatamatika juni 30 mwaka 2026.
Man City tayari wamekamilisha mazungumzo binafsi na mchezaji kilichobaki ni kusubiri endapo ofa rasmi waliyoiwasilisha kwa klabu Lyon itakubaliwa ili wajihakikishie huduma ya mchezaji huyo msimu ujao.