Manchester City wakubali kumsajili Sávio kutoka Girona
Eric Buyanza
February 6, 2024
Share :
Haya yamewekwa wazi na gwiji wa habari za uhamisho wa kandanda duniani, Fabrizio Romano kupitia tweet yake siku ya jana (Jumatatu).
"Manchester City imekubali kumsajili Sávio kutoka Girona msimu wa joto..Hati zitatiwa saini katika siku chache zijazo." Aliandika Romano.
Aliongeza kwasasa Mbrazil huyo ata-focus na klabu yake ya Girona hadi mwisho wa msimu kabla ya kuondoka kwenye msimu wa joto.
Kulingana na Romano, mabingwa hao wa Premier League walishinda mbio za kumsajili fowadi huyo mwenye umri wa miaka 19 licha ya ombi kutoka kwa vilabu vya Ujerumani na Uingereza.