Manchester United kufuata ushauri wa Roy Keane, wamtaka Watkins
Eric Buyanza
May 16, 2024
Share :
Manchester United wanafikiria kuchukua ushauri wa Roy Keane kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa, Ollie Watkins.
Akiongea mwezi uliopita Keanea alinukuliwa akisema, “mfungaji huyo bora wa Villa anaweza kuja kucheza klabu moja kubwa kama Manchester au Liverpool” baada ya kumshuhudia akifunga mabao 19 msimu huu.
Sasa inaonekana kama Man U wameamua kuufanyia kazi ushauri wa Roy baada ya kuanza michakato ya kumnasa mshambuliaji huyo tegemeo wa Aston Villa.