Manchester United wafanya mazungumzo na wakala wa Adrien Rabiot
Eric Buyanza
May 4, 2024
Share :
Manchester United wanataka kumsajili Adrien Rabiot kama mchezaji huru mwishoni wa msimu huu.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka TEAMtalk, Manchester United wamekuwa wakiwasiliana na wakala wa kiungo huyo... lakini wanakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa klabu za PSG, Barcelona na Bayern Munich kwenye kuiwania saini yake.