Manchester United wanaitaka saini ya Tosin Adarabioyo
Eric Buyanza
May 10, 2024
Share :
Manchester United wameingia kwenye mbio za kumnasa beki wa kati wa klabu ya Fulham,Tosin Adarabioyo.
ESPN inaripoti kwamba muingereza huyo anaweza kuhamia Old Trafford kama mchezaji huru.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City mwenye umri wa miaka 26 yumo kwenye orodha ya wachezaji wanaoangaliwa kwa umakini na vilabu kadhaa vya Uingereza, huku vilabu kama Newcastle, Chelsea, na Tottenham wakionyesha nia ya kumnunua.
Muingereza huyo alikataa kuongezewa mkataba na Fulham mapema mwaka huu na hivi majuzi alitemwa na meneja Marco Silva.