Manchester united yamtangaza Mkurugenzi mpya wa Ufundi
Eric Buyanza
April 20, 2024
Share :
Manchester United imethibitisha kumteua Jason Wilcox kama mkurugenzi wao mpya wa ufundi, ikiwa ni muendelezo wa marekebisho yanayofanywa na Sir Jim Ratcliffe.
Wilcox mwenye umri wa miaka 53, anaacha nafasi yake kama mkurugenzi wa soka katika klabu ya Southampton na ataanza wadhifa wake mpya Old Trafford mara moja baada ya klabu hizo mbili kufikia makubaliano kuhusu fidia.
Atafanya kazi na maeneo yote ya kiufundi ya idara ya soka.