pmbet

Manchester United yapata pigo kubwa kuelekea game yao na Aston Villa

Eric Buyanza

February 6, 2024
Share :

Manchester United imethibitisha kuwa Lisandro Martínez atakuwa nje kwa miezi miwili kutokana na jeraha la goti.
 

Martinez alilazimika kutolewa nje kipindi cha pili cha ushindi wao wa 3-0 dhidi ya West Ham Jumapili.
 

Beki huyo wa Argentina alifanyiwa vipimo Jumatatu na anatarajiwa kukosa wiki nane zijazo.
 

"Lisandro Martínez amepata jeraha kwenye mishipa ya kati kwenye goti lake na anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa angalau wiki nane.
 

“Beki huyo wa Argentina aliondoka uwanjani katika dakika ya 71 ya ushindi wetu wa 3-0 dhidi ya West Ham United Uwanja wa Old Trafford Jumapili. Sote tunamuombea apate nafuu ya haraka na tunatazamia kumuona akirejea uwanjani baadaye msimu huu,” taarifa rasmi kutoka United ilisema.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet