Mandonga vitani usiku wa leo
Eric Buyanza
December 29, 2023
Share :
Bondia mwenye kila aina ya vituko Karim Mandonga leo Desemba 29, 2023 atapanda ulingoni kuzichapa na Jiti Mawe katika pambano lilopewa jina la #UsikuWaVisasi.
Hakika utakua ni usiku wa kihistoria kwa wapenzi wa ngumi Morogoro ambapo pamabano hilo litafanyika kwenye ukumbi wa Tanzanite.
Mabondia kutoka Morogoro na maeneo mengine watapanda ulingoni pia kwa ajili ya kutoa hamasa kwa vijana wenye ndoto ya kuishi katika mchezo wa masumbwi.
Kama kawaida yake, Mandonga amemmchimba mkwara mzito mpinzani wake ya kwamba atamgalagaza mapema kabisa kwenye pambano hilo akitumia ngumi mpya aliyoitambulisha kwa jina la 'Chifu Kingalu