Mane asimulia alivyoikataa Man Utd
Sisti Herman
November 21, 2025
Share :

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Sadio Mane amefichua kuwa alikataa ofa ya kujiunga na Manchester United na badala yake kuhamia Liverpool kwa sababu hakushawishika na uhakika wa kocha Louis van Gaal wa kumpa muda wa kucheza.
Mane alijiunga na The Reds kwa Pauni Milioni 30 ambazo ni sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni 90 za Kitanzania mwaka 2016, na alicheza mechi 269, akifunga mabao 120.
Aliunda uhusiano wa kutisha na wachezaji kama Mohamed Salah na Roberto Firmino kabla ya kwenda Bayern Munich mnamo 2022.
Kabla ya kuhamia Liverpool, hata hivyo,kulikuwa na hamu kubwa ya huduma yake kutoka United, lakini uhamisho haukufanyika.
Akizungumzia hali hiyo, Mane amefichua kuwa kulikuwa na mawasiliano kutoka United, lakini akachagua kutohamia Old Trafford kwa sababu ya van Gaal.
"Manchester United walinipigia simu wakati huo, "Nilikuwa nikizungumza na van Gaal wakati huo. Wayne Rooney alikuwepo. Na Angel Di María alikuwepo. Na Memphis Depay alikuwepo, Alisema Mane.
Uzito wa Kikosi cha United wakati huo ulimpa hofu Msenegali huyo na kujikuta anavaa uzi mwekundu wa Liverpool.





