Mange Kimambi na Mashabiki wampelekea moto Tanasha Dona anyoosha mikono.
Joyce Shedrack
March 11, 2025
Share :
Mwanamuziki kutoka Kenya Tanasha Dona ambaye pia ni mzazi mwenza kwa Diamond Platnumz ameamua kufata ushauri kutoka kwa mashabiki zake kuhusiana na muonekano wa midomo yake ya chini yaani 'lips' ambazo aliziongeza na kufanya ziwe nene tofauti na alivyozaliwa.
Kupitia ukurasa wake wa snapchat Tanasha amesema kuwa: "Sawa nitaziyeyusha fillers zilizopo kwenye lip zangu, mmeshinda"
Hii pia imechagizwa na kukosolewa na Mwanadada Mange Kimambi kupitia Snapchat akimtaka arudi tu kama alivyokuwa kwasababu yeye ni Mremboo na hakuwa na haja ya kufanya 'Surgery'