Manqoba asema hana presha na kazi yake Yanga.
Joyce Shedrack
September 14, 2026
Share :
Kocha wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi, amesema hana presha na anaendelea kufurahia ushindani wa ligi, akisisitiza kuwa bado kuna safari ndefu na mechi nyingi muhimu mbele yao. “Sina presha, niko kwenye nafasi ambayo nilitamani kuwa.
Tunapaswa kufurahia ushindani na kuona mapambano yataishia wapi. Hii ni ligi yenye ushindani mkubwa na bado hatujacheza dhidi ya baadhi ya timu kubwa, hivyo tunapaswa kuchukua mchezo mmoja baada ya mwingine.
Bado kuna mambo mengi tunapaswa kuyaboresha. Tatizo ni kwamba tunapokosa muda wa kutosha wa mazoezi, inakuwa vigumu kufanya maboresho makubwa. Tunatumaini mapumziko ya FIFA yatatusaidia kwa kiasi fulani, ikiwemo kuboresha viwango vya utimamu wa baadhi ya wachezaji.





