Manula ageukia biashara sasa, azindua duka la vifaa vya michezo
Sisti Herman
March 17, 2024
Share :
Kipa namba moja wa klabu ya Simba na timu ya Taifa Tanzania, Aishi Manula ameamua kuwekeza kibiashara nje ya uwanja baada ya leo kuzindua duka lake la vifaa vya michezo liitwalo "AIR MANULA SPORTS STORE".
Akizungumza na PM Sports Manula amesema jina hilo limetoholewa kwenye neno "AIR MANULA" ambalo ni jina lake la utani kutokana na utambulisho huo ameamua kulitumia kama chapa ya kibiashara.
Duka hilo la Manula lipo mitaa ya Kinondoni Morocco, jijini Dar es Salaam.