Manula atembelea taasisi ya tiba asili Muhimbili
Sisti Herman
October 23, 2025
Share :

Reposted from @dawaasili_muhimbili
Leo tumemkaribisha Aishi Salum Manula, golikipa wa Azam FC na Taifa Stars, katika Taasisi ya Dawa Asili (ITM) ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Manula alipita katika duka la bidhaa za Dawa Asili na kupata fursa ya kufahamu bidhaa mbalimbali za Taasisi, huduma kwa jamii, na pia kuchukua bidhaa kwa matumizi yake binafsi.
Aidha, alikutana na Mkurugenzi wa ITM kwa mazungumzo ya kina kuhusu nafasi ya tiba asili katika afya ya jamii.
Baadaye, alitembelea Dawati la Taarifa (Information Desk) la MUHAS sehemu mpya kwa wageni kupata taarifa zote za chuo na kujionea sehemu ya maonesho ya bidhaa za MUHAS iliyopo hapo.
Tunampongeza kwa unyenyekevu, udadisi na hamasa yake ya kufahamu urithi wa tiba asili wa Tanzania, na pia tunamkaribisha tena MUHAS wakati wowote! Aishi





