Maombi yaanze leo....! MC Alger na TP Mazembe kinapigwa Algeria.
Joyce Shedrack
January 10, 2025
Share :
Ligi ya Mabingwa barani Afrika inaendelea siku ya leo ambapo wapinzani wa klabu ya Yanga kwenye michuano hiyo watashuka dimbani Nchini Algeria MC Alger akiwa nyumbani dhidi ya TP Mazembe majira saa 4:00 usiku.
Mchezo huo wa kundi A unawakutanisha MC Alger waliopo nafasi ya 2 kwenye msimamo wa kundi A akiwa na alama 5 baada ya kucheza mechi 4 huku TP Mazembe akiwa na alama 2 baada ya kucheza michezo 4 katika michuano hiyo.
MC Alger akishinda mchezo huo ataendelea kujikita nafasi ya pili kwenye msimamo huo akiwa amekusanya alama 8 huku akibakiwa na mchezo wa mwisho ugenini dhidi ya Yanga kwenye dimba la Benjamini Mkapa utakaoamua nani afuzu hatua ya makundi endapo Yanga atafanikiwa kupata alama 3 dhidi ya AL Hilal siku ya jumapili.