Mapambano yaongezeka mashariki ya Kongo
Eric Buyanza
June 29, 2024
Share :
Mapigano yameongezeka katika mji wa kimkakati mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23.
Makabiliano ya jana Ijumaa yalitokea katika mji wa Kanyabayonga, ulioko kaskazini mwa uwanja wa mapambano katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Mji wa Kanyabayonga unachukuliwa kuwa mlango wa kuingia Butembo na Beni katika upande wa kaskazini, ambazo ni ngome za kabila la Nande na vituo muhimu vya kibiashara.
Kanyabayonga, ni mji wenye wakazi 60,000, na uko karibu kilomizta 100 kutoka mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Goma, ambao pia umezingirwa na waasi hao wanaoungwa mkono na Rwanda. DW imeripoti kuwa waasi wa M23 walisonga mbele kuelekea Kanyabayonga katika wilaya ya Lubero, ikiwa ni eneo la nne la mkoa huo, ambalo kundi hilo limeingia.