Mapema tu nyota zao zimeanza kung'aa kwa Ancelotti.
Joyce Shedrack
May 28, 2025
Share :
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Brazil Carlo Ancelotti amewarejesha kwenye kikosi cha Timu ya Taifa wachezaji wawili waliokosekana kwenye timu hiyo kwa muda mrefu kiungo Carlos Henrique Casemiro pamoja na Antony Matheus dos Santos wa Real Bettis.

Casemiro ambaye alipigwa chini katika majukumu ya Timu ya Taifa tangu mwaka 2023 huku Antony akikosekana kwenye majukumu ya Taifa lake tangu mwaka 2022.
Kikosi hicho kilichoitwa na Ancelotti aliyekabidhiwa majukumu ya kuifundisha Timu ya Taifa kwa mara ya kwanza ni kwa ajili ya michezo miwili ya kufuzu Kombe la Dunia itakayopigwa mwezi wa sita dhidi ya Ecuador na Paraguay.