Mapenzi katika umri mdogo, na kuwa na wapenzi wengi chanzo cha saratani
Eric Buyanza
April 24, 2024
Share :
Imeripotiwa kuwa asilimia nane ya wanawake wa Mkoa wa Kigoma waliofanyiwa uchunguzi wa awali wa saratani ya mlango wa kizazi kwa mwaka 2023 wamegundulika kuwa na viashiria vya ugonjwa huo.
Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Jesca Leba katika uzinduzi wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana kati ya umri wa miaka tisa hadi 14 uliofanyika katika sekondari ya Msimba iliyopo halamsahauri ya wilaya ya Kigoma.
Mganga Mkuu ametaja sababu za kuenea kwa ugonjwa huo kuwa ni pamoja kufanya mapenzi katika umri mdogo, kunywa pombe kali, kuvuta sigara na kuwa na mahusiano na watu wengi.
NIPASHE