pmbet

Mapigano yazidi kongo silaha nzito zatumika

Eric Buyanza

March 28, 2026
Share :

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linasema, mapigano Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameongezeka maradufu huku matumizi ya silaha nzito na ndege zisizo na rubani yakihatarisha maisha ya raia.
 

Licha ya kuondoka kwa waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda kutoka kwenye mji wa Uvira, mapigano bado yanapamba moto kwenye maeneo ya Kivu Kaskazini na Kusini.
 

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Vivian Van De Perre ametahadharisha kwamba,hali ya usalama huko Kivu Kusini bado ni tete, na mapigano mapya yanaongezeka na kuelekea kwenye mpaka kati ya Kongo na Burundi hali ambayo inaongeza hatari ya kuzuka kwa mgogoro wa kikanda.

 

DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet