pmbet

MAPINDUZI KWENYE SOKA: Mwamuzi Uruguay atumia kadi za kidijitali

Eric Buyanza

October 17, 2026
Share :

Mapinduzi ya kidijitali yameingia rasmi uwanjani nchini Uruguay, baada ya mwamuzi wa soka kufanya historia kwa kutumia kifaa cha kielektroniki badala ya kadi za kawaida za makaratasi kutoa adhabu za kadi ya manjano na nyekundu.

 

Tukio hilo la kihistoria lilifanyika Alhamisi iliyopita wakati wa mechi ya Copa Uruguay kati ya timu za Nacional na Rentistas katika uwanja wa Gran Parque Central, Montevideo. Mwamuzi Eduardo Varela alionekana akionyesha kifaa chenye ukubwa wa simu janja (smartphone), ambacho kikibonyezwa huwaka rangi ya manjano au nyekundu kuashiria adhabu.

 

Katika mchezo huo kiungo wa Rentistas, Juan Pablo Plada, aliingia kwenye vitabu vya historia kama mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya manjano ya kidijitali katika dakika ya 12.

Ingawa teknolojia hii imeonekana kurahisisha kazi ya kiutawala kwa waamuzi, bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya uonaji (visibility).

 

Majaribio ya awali ya mchana yalifutwa kwa sababu mwanga wa jua ulifanya kioo kisionekane vyema. Hata kwenye mechi hiyo ya usiku, mashabiki uwanjani na watazamaji wa runinga walipata shida kutofautisha rangi zilizowaka kwenye kifaa hicho. Waendelezaji wa teknolojia hiyo wamesema wanafikiria kuweka taa za LED pembezoni mwa kioo ili kuongeza mwangaza.

Kwa sasa mfumo huu bado uko kwenye awamu ya majaribio, lakini wabunifu wake wana matumaini kuwa baada ya maboresho, unaweza kupitishwa na Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (CONMEBOL) pamoja na FIFA.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet