MAPINDUZI YA ZIDANE: Ganiou aitwa kikosi cha awali dhidi ya Uturuki
Eric Buyanza
September 12, 2026
Share :

Mapinduzi ya Zinedine Zidane ndani ya benchi la ufundi la timu ya taifa ya Ufaransa yameanza kwa kishindo. Kocha huyo amemjumuisha beki chipukizi wa RC Lens, Ismaïlo Ganiou, katika kikosi chake cha awali chenye wachezaji 50.
Ganiou, mwenye umri wa miaka 21, amekuwa mhimili mkubwa wa safu ya ulinzi ya Lens msimu huu.
Hatua hii imekuja kabla ya tangazo rasmi la kikosi cha mwisho litakalotolewa Ijumaa, Septemba 18.
Kikosi hiki kinajiandaa na ratiba ngumu ya michuano ya UEFA Nations League, ambapo mechi ya kwanza itakuwa dhidi ya Uturuki tarehe 25 Septemba.
Beki tegemeo wa Arsenal, William Saliba, hatakuwepo katika kambi hii kutokana na majeraha, jambo lililomlazimu Zidane kutafuta mbadala wa haraka.
Lakini pia Ganiou alionyesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo wake wa kwanza wa UEFA Champions League hivi karibuni, akiiwezesha Lens kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Slavia Prague.
Zidane alikuwepo jukwaani akimtazama beki huyo wakati wa mchezo wa Champions Trophy dhidi ya Paris Saint-Germain na kuridhishwa na uwezo wake.





