Mara ya mwisho kuvuta na Snoop, nilipoteza uwezo wa kuona - Ed Sheeran
Eric Buyanza
April 25, 2025
Share :
Mwanamuziki wa Uingereza, Ed Sheeran ameeleza kuwa aliwahi kupoteza uwezo wa kuona kwa muda baada ya 'kusmoke' na rapa nguli wa Marekani, Snoop Dogg.
Kupitia ukurasa wake wa TikTok hapo jana, Sheeran alipost video akiwa na Snoop Dogg, huku Rapa huyo akionekana akiwa ananyonga kitu kwenye mikono yake.
Chini ya video hiyo Ed Sheeran akaandika "Mara ya mwisho kuvuta na Snoop nilipoteza uwezo wa kuona."