pmbet

Marc Cucurella kuchora Tattoo yenye sura ya kocha Luis De La Fuente

Eric Buyanza

July 20, 2026
Share :

Beki wa Hispania, Marc Cucurella, anataka kuchora tattoo ya uso wa kocha Luis de la Fuente kutokana na ahadi aliyoiweka kabla ya fainali ya Kombe la Dunia la 2026.

 

Cucurella aliahidi kuwa ikiwa timu ya taifa ya Hispania ingefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Argentina, basi angejichora tattoo ya sura ya kocha wake kama ishara ya kumuenzi na kusherehekea mafanikio hayo ya kihistoria.

 

Baada ya Hispania kufanikiwa kushinda fainali hiyo kwa goli 1-0 Cucurella amethibitisha kuwa atatimiza ahadi hiyo na amepanga kuichora tattoo hiyo kwenye sehemu ya mwili inayoonekana.

 

Kabla ya hapo, Cucurella alishawahi kutimiza ahadi nyingine ya kupaka nywele zake rangi nyekundu baada ya Hispania kutwaa ubingwa wa Euro 2024.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet