Marcus Rashford sasa kwenye rada za Juventus
Eric Buyanza
July 17, 2025
Share :
Sky Sports Italia, wanaripoti kuwa Juventus wanavutiwa na Marcus Rashford, na tayari wameanza kuchunguza mazingira na uwezekano wa kupata huduma ya fowadi huyo wa Manchester United.
Taarifa zinasema Barcelona pia wana nia na mchezaji huyo lakini bado hawajaonyesha jitihada zozote mpaka sasa.
Rashford amewahi kuzungumza hadharani kuhusu nia yake ya kuichezea Barcelona.
#TetesiZaSoka