pmbet

Marekani imeshindwa kama mpatanishi mzozo wa DRC - M23

Eric Buyanza

May 11, 2026
Share :

Waasi wa AFC/M23 wamesema Marekani imeshindwa kutekeleza ipasavyo wajibu wake kama mpatanishi katika juhudi za kukomesha mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
 

Kiongozi wa waasi hao Corneille Nangaa alimwandikia barua Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio na kumueleza kuwa Washington imeshindwa kuiwajibisha serikali mjini Kinshasa kuhusu madai ya ukiukaji wa makubaliano ya amani.

 

Katika barua hiyo, Nangaa amelaani hatua ya Marekani kuwawekea vikwazo watu wanaoikosoa serikali mjini Kinshasa, kauli iliyoashiria vikwazo alivyowekewa wiki iliyopita,  rais wa zamani wa Kongo Joseph Kabila  kwa madai ya kuwafadhili waasi hao.
 

Licha ya DRC na Rwanda kusaini makubaliano ya washington mwaka 2025, mapigano yanaendelea kusababisha maafa makubwa mashariki mwa Kongo, huku pande zote mbili zikituhumiana kukiuka makubaliano hayo.


 

DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet