Marekani itashindwa kuikoa Israel kama tutachokozwa - Iran
Eric Buyanza
July 5, 2025
Share :
Mkuu wa Majeshi ya Iran Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi ameapa kuwa vikosi vya ulinzi vitatoa jibu la “mapigo ya kupoozesha” kwa uchokozi mwingine wowote mpya wa kijeshi utakaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel; na akaonya kwamba, mapigo hayo yatakuwa makali kiasi cha kuifanya hata Marekani ishindwe kumuokoa Netanyahu.
Akihutubia hafla iliyofanyika mjini Tehran, Jenerali Mousavi amesema, Jamhuri ya Kiislamu ilikuwa imeandaa jibu hilo dhidi ya uchokozi uliofanywa Israel kwa kufuata agizo lililotolewa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
“Hata hivyo haikupatikana fursa ya kulitekeleza”, ameeleza kamanda huyo huku akisisitiza kuwa bila shaka yoyote taifa la Iran litatoa jibu hilo endapo Israel itafanya uchokozi mwingine.
“Kama wataishambulia tena Iran, wataona tunayoweza kuyafanya. Katika hali hiyo, hata Marekani yamkini itashindwa kumuokoa Netanyahu”.