pmbet

Marekani kudhibiti mapipa Bilioni 65 ya mafuta ya Venezuela

Eric Buyanza

August 29, 2026
Share :

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema wamefikia makubaliano ya mafuta na Venezuela, hatua ambayo itaongeza zaidi ya mara mbili akiba ya mafuta ya Marekani, kuongeza upatikanaji wa mafuta na kushusha bei za petroli.

 

“Kwa maelekezo yangu, Waziri wa Mambo ya Nje, Marco Rubio na Waziri wa Vita, Pete Hegseth, wakishirikiana kwa karibu na Rais wa Mpito wa Venezuela anayeheshimika sana, Delcy Rodríguez, pamoja na kupitia ushirikiano na sekta binafsi, wamefanikisha udhibiti wa sehemu kubwa wa Marekani wa zaidi ya mapipa bilioni 65 ya akiba ya mafuta iliyothibitishwa nchini Venezuela, bila gharama yoyote kwa mlipakodi wa Marekani,” Trump ameandika kwenye mitandao ya kijamii.
 

Msisitizo wa Trump kuhusu kushusha bei ya petroli nchini Marekani, ikiwa imesalia karibu miezi miwili kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula, unakuja wakati wastani wa kitaifa wa bei ya petroli ukiwa zaidi ya Dola nne za Marekani kwa galoni.

 

Makubaliano hayo yamekuja wakati ambao vita vya Iran vimevuruga sehemu ya tano ya usambazaji wa mafuta duniani kwa kipindi cha miezi sita.
 

“Hatua hii ya kihistoria inaongeza zaidi ya mara mbili akiba ya mafuta ya Marekani, unaongeza kwa kiasi kikubwa usambazaji wetu wa mafuta na utashusha kwa kiasi kikubwa bei za petroli kwa Wamarekani wote kwa muda mrefu ujao, huku ukisaidia kuendelea kuiweka Venezuela katika njia ya mafanikio makubwa na ustawi mkubwa,” Trump ameandika katika ujumbe wake.
 

Rais Rodríguez pia amesifu makubaliano hayo kati ya nchi hizo mbili.
 

“Lengo letu ni kuelekea katika kuimarisha nafasi yetu kama taifa lenye nguvu katika uzalishaji wa nishati, kwa kuweka akiba yetu kubwa ya mafuta katika huduma ya maendeleo ya kitaifa, uanzishaji wa ajira, ongezeko la kipato kwa wafanyakazi wetu na ustawi wa wananchi wetu,” amesema katika taarifa yake ya jana usiku.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet