Marekani kuipa tena Ukraine mitambo ya kudungua makombora
Eric Buyanza
June 13, 2024
Share :
Tangazo la kutumwa kwa zana za kisasa za vita kwenda Ukraine, linakuja wakati huu ambapo rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekua akitoa wito kwa mataifa washirika kuisaidia nchi yake vifaa zaidi vya ulinzi wa anga.
Zelensky amekuwa akitaka kuimarisha zaidi ulinzi wa anga la nchi hiyo haswa katika mji wa Kharkiv mashariki mwa Ukraine ambapo wanajeshi wa Urusi wameripotiwa kuzidisha kasi ya mashambulizi katika siku za karibuni.
Kwa mujibu wa gazeti la The New York Times, mitambo hiyo ya ulinzi wa angani kutoka Marekani kwa sasa ipo nchini Poland ikiwa inaelekea Ukraine .
Washirika wengine wa Ukraine kutoka nchi za Magharibi akiwemo Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz , amekuwa akitoa wito wa kuisaidia Ukraine kuimarisha zaidi ulinzi wake wa anga.
Ujerumani tayari imeipa Ukraine vifaa vitatu vya kudungua makombora angani.
RFI