Marekani kupeleka Ukraine mfumo wa makombora ya Patriot
Eric Buyanza
April 27, 2024
Share :
Marekani imesema itaharakisha kupeleka makombora ya ulinzi wa anga ya Patriot na risasi za kivita nchini Ukraine kama sehemu ya msaada wa kijeshi.
Hata hivyo mifumo ya Patriot ya kurusha makombora haitatumwa, Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin alisema.
Hivi karibuni Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema Patriot inahitajika "haraka" kukabiliana na tishio la anga la Urusi na "wanapaswa kuokoa maisha" haraka iwezekanavyo.
Leo Jumamosi, Ukraine imenukuliwa ikisema Urusi imefanya shambulio kubwa la anga na kuharibu Hospitali.