Marekani kuwanyima silaha Ukraine!
Eric Buyanza
December 6, 2023
Share :
Mkurugenzi wa Ofisi ya Usimamizi na Bajeti ya Ikulu ya Marekani (White House) Shalanda Young, amesema kuwa Marekani haitaweza kuendelea kutoa silaha na vifaa zaidi kwa Ukraine ikiwa Bunge la Congress halitaidhinisha (halitakubali) ufadhili wa ziada mwishoni mwa mwaka huu.
Ufadhili wa Marekani kwa Ukraine unaisha mwishoni mwa mwaka huu 2023, hivyo Bunge la Marekani la Congress linapaswa kukubali kupitisha bajeti nyingine kwaajili ya kuendelea kutoa msaada wa silaha kwa Ukraine.
Kwa wiki kadhaa Ikulu ya Marekani (White House) imekuwa ikiliomba Bunge la Congress kuchukua hatua ya haraka juu ya ombi lake la nyongeza za fedha, ikisema kwamba kutofanya hivyo kunaweza kuhatarisha maendeleo ya Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi.
"Kukata utiririshaji wa silaha na vifaa vya Marekani kutaifunika Ukraine kwenye uwanja wa vita," Shalanda Young, mkurugenzi wa Ofisi ya Usimamizi na Bajeti ya Ikulu ya White House, aliandika katika barua kwa Spika wa Bunge Mike Johnson.
(Chanzo: Wall Street Journal)