pmbet

Marekani kuwauzia Saudi Arabia silaha zenye thamani ya Trilioni 13

Eric Buyanza

September 5, 2026
Share :

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetangaza kuidhinisha makubaliano ya kuiuzia Saudi Arabia silaha zenye thamani ya dola bilioni 5 (takriban Shilingi za Kitanzania trilioni 13 na bilioni 237).

 

Katika taarifa, wizara hiyo imesema imeidhinisha ombi la Saudi Arabia la kununua maelfu ya mabomu pamoja na mifumo ya kuongoza makombora ya masafa marefu.

 

Kwa mujibu wa wizara hiyo, makubaliano hayo pia yanajumuisha silaha mbalimbali, vipuri na kemikali, pamoja na huduma za kiufundi na kimkakati za usafirishaji na ugavi.

 

Marekani imesema makubaliano hayo yanalenga kuimarisha usalama wa mshirika wake muhimu, huku yakisaidia kudumisha utulivu wa kisiasa na maendeleo ya kiuchumi katika eneo la Ghuba.

 

Wizara hiyo imeongeza kuwa makubaliano hayo yataimarisha uwezo wa Saudi Arabia wa kujilinda dhidi ya mashambulizi ya anga na kukabiliana na vitisho vinavyoikabili eneo hilo.

 

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet