pmbet

Marekani na Saudia wapeleka mashambulizi nchini Iraq

Eric Buyanza

July 29, 2026
Share :

Vikosi vya Marekani na Saudi Arabia vimesema vimewashambulia wanamgambo wa Iraq wenye mahusiano na Iran, kujibu mashambulizi ya karibuni baada ya usitishwaji wa muda mfupi wa mapigano kwenye vita vya Iran.
 

Mashambulizi hayo ya kulipa kisasi yalivilenga vituo vya usafirishaji wa vifaa na maghala ya silaha mashariki mwa Iraq, vinavyomilikiwa na wanamgambo hao ambao Marekani inasema ni "makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Iran.”

 

Wizara ya Ulinzi ya Saudi Arabia imesema magaidi hao wanahusishwa na mashambulizi dhidi ya miundombinu ya mafuta nchini humo.

 

Mashambulizi hayo ya pamoja ya angani yanafanyika wakati ambapo Rais Donald Trump amekutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Washington kwa mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana tangu kuanza kwa vita vya Iran katikati ya mwezi Februari.
 

DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet