Marekani yaituhumu China kwa kufanya jaribio la siri la nyuklia
Eric Buyanza
February 19, 2026
Share :
Shutuma za Marekani dhidi ya China zinafufua mvutano kati ya mataifa yenye nguvu za nyuklia na kufufua mjadala kuhusu mustakabali wa udhibiti wa silaha, dhidi ya hali ya ushindani mkubwa wa kimkakati na kutokuaminiana kunakoongezeka kati ya mataifa yenye silaha za nyuklia.
Marekani inadai kuwa na ushahidi kwamba China ilifanya jaribio la siri la nyuklia, ishara ya matetemeko ya ardhi iliyogunduliwa mnamo mwezi Juni 2020 karibu na eneo la Lop Nur magharibi mwa China inaedana na mlipuko wa nyuklia wenye nguvu ndogo.
Mamlaka ya Marekani inaamini data zilizorekodiwa hazihusiani na tetemeko la ardhi la asili au shughuli yoyote ya uchimbaji madini huku ikiamini kulikuwa jaribio la siri lililofanyika kwa makusudi. Hata hivyo China imepuuza shutuma hizo na kuilaumu Marekani kwa kupotosha ukweli.
Wataalam wa siasa za dunia wanasema kuna uwezekano mkubwa kwa Marekani nayo kufanya majaribio yake ya nyuklia, kulipa kile walichokifanya China ili kuweka usawa.






