pmbet

Marekani yamzuia kiongozi wa Palestina kuingia New York

Eric Buyanza

August 30, 2025
Share :

Marekani imesema haitamruhusu Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas kwenda New York nchini Marekani mwezi ujao kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa.

Abbas amezuiwa kuhudhuria mkutano huo baada ya yeye na maafisa wengine 80 wa Palestina kufutiwa Viza zao, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha.

Ofisi ya Abbas ilisema imesikitishwa na uamuzi huo wa kumnyima viza, ambao "unapingana waziwazi na sheria za kimataifa na Mkataba wa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, na kuitaka Marekani kubadili uamuzi huo.

Chini ya "makubaliano ya makao makuu" ya Umoja wa Mataifa ya 1947, Marekani kwa ujumla inahitajika kuruhusu wanadiplomasia wa kigeni kuingia Umoja wa Mataifa huko New York.

Marekani hata hivyo, imesema inaweza kukataa visa kwa sababu za kiusalama, itikadi kali na sera za kigeni.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet