pmbet

Marekani yapanga kupeleka wanajeshi wa ardhini nchini Iran

Eric Buyanza

March 21, 2026
Share :

Maafisa wa jeshi la Marekani wanafanya maandalizi ya kina wa kupeleka wanajeshi wa ardhini nchini Iran, kwa mujibu wa mshirika wa BBC nchini humo (CBS News), ikinukuu vyanzo kadhaa visivyotajwa majina vilivyofahamishwa kuhusu mjadala huo.

Maafisa waandamizi wa Pentagon wanatoa maombi maalum ya kupanga hatua kama hiyo, CBS inaripoti.
 

Mipango hiyo pia inajumuisha mazungumzo kuhusu jinsi Marekani itakavyoshughulikia kuwashikilia wanajeshi wa Iran iwapo wanajeshi wa Marekani watakuwa nchini humo, kulingana na maafisa wawili walionukuliwa.

 

Siku ya Ijumaa, Rais Donald Trump alisema kuwa Marekani ilikuwa inazingatia “kupunguza” operesheni zake dhidi ya Iran. Hapo awali aliwaambia waandishi wa habari kwamba hataki kusitisha mapigano.
 

Pia alisema kuwa hana mpango wa kupeleka wanajeshi wa ardhini “mahali popote,” akiongeza: “Kama ningekuwa na mpango huo, bila shaka nisingewaambia.”

Wizara ya Ulinzi haijajibu ombi la BBC la kutoa maoni kuhusu taarifa hizo za uwezekano wa kupelekwa kwa wanajeshi.
 

Kamandi kuu ya jeshi, inayosimamia operesheni za kijeshi za Washington katika Mashariki ya Kati, ilikataa kuzungumza kuhusu uwezekano wa hatua hizo.


 

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet