Marekani yasitisha msaada wa mabomu kwa Israel
Eric Buyanza
May 8, 2024
Share :
Marekani ilisitisha usafirishaji wa mabomu kwenda Israel wiki iliyopita baada ya serikali ya Benjamin Netanyahu kushindwa kushughulikia wasiwasi wa Marekani kuhusu mpango wake wa kuuvamia mji wa Rafah, ulioko kusini mwa Gaza.
Afisa mwandamizi katika utawala wa Rais Joe Biden, akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, ameeleza kuwa Marekani ilizuia usafirishaji wa shehena ya mabomu kwenda Israel wiki iliyopita.
Afisa huyo ameongeza kuwa bado hawajafanya uamuzi kuhusu iwapo wataendelea na usafirishaji wa silaha hizo.
Miongoni mwa sialha hizo ni mabomu yenye uzito wa kilogram 900, na kilogram 225.
Utawala wa Biden ulifanya uamuzi wa kuzuia usafirishaji wa shehena hiyo ya silaha baada ya Israel kuonekana kuwa tayari kuendelea na oparesheni kubwa ya kijeshi mjini Rafah, operesheni ambayo imepingwa vikali na Marekani.
VOA