Marekani yatangaza vikwazo vipya zaidi ya 500 kwa Urusi
Eric Buyanza
February 24, 2024
Share :
Serikali ya Marekani imetangaza vikwazo vipya zaidi ya 500 dhidi ya Urusi kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine na kifo cha kiongozi wa upinzani Alexei Navalny.
Vikwazo hivyo vinawalenga watu waliohusishwa na kifungo cha Navalny na taasisi zinazoongoza vita vya Urusi dhidi ya Ukraine Rais Joe Biden amesema.
Pia vikwazo vya kuuza bidhaa nje vitawekwa kwa karibu makampuni 100.
EU pia ilitangaza vikwazo, ambavyo Moscow ilijibu kwa kupiga marufuku maafisa wa EU kuingia Urusi.
Haijulikani ni athari gani vikwazo hivyo vitaleta kwa uchumi wa Urusi.
Vikwazo hivyo vinakuja wiki moja tangu Navalny kufariki ghafla katika jela ya Arctic Circle. Bwana Biden amesema "hakuna shaka" rais wa Urusi ndiye anayepaswa kulaumiwa.