Marekani yathibitisha kuuawa kwa kiongozi wa Hamas (Marwan Issa)
Eric Buyanza
March 19, 2024
Share :
Kiongozi wa Hamas Marwan Issa alifariki katika shambulizi la anga la Israel, afisa wa Ikulu ya Marekani Jake Sullivan amethibitisha.
Akiwa naibu kamanda wa kijeshi, Bw Issa atakuwa kiongozi mkuu wa Hamas kufariki tangu vita vilipoanza tarehe 7 Oktoba.
Hata hivyo Kundi la Wapalestina, linalodhibiti Gaza, halijazungumzia rasmi ripoti za kifo chake.
Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa Bw Issa aliuawa katika shambulizi la anga lililolenga eneo la chini ya kambi ya wakimbizi ya Nuseirat katikati mwa Gaza wiki moja iliyopita.
BBC