Marekani yazuia meli nyingine ya Iran
Eric Buyanza
April 25, 2026
Share :

Jeshi la Marekani limesema limefanikiwa kuizuia meli nyingine iliyokuwa na bendera ya Iran ikiwa njiani kuelekea bandari ya Iran, kama sehemu ya hatua za kuimarisha mzingiro wa baharini dhidi ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka jeshi la nchi hiyo, operesheni hiyo ilifanyika Aprili 24, ikiongozwa na manowari ya kivita ya USS Rafael Peralta, ambayo ilitekeleza hatua za kudhibiti usafiri wa majini unaohusishwa na Iran.
Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi pana za Marekani za kuzuia biashara ya mafuta ya Iran na kukata vyanzo vya mapato ya nchi hiyo, hasa kufuatia mvutano unaoendelea kati ya pande hizo mbili.
Mvutano huo umeongezeka katika wiki za karibuni baada ya Marekani kufanya mashambulizi ya kijeshi na Iran kujibu kwa kuzuia baadhi ya njia muhimu za usafirishaji wa mafuta katika eneo la mlango bahari wa Hormuz, jambo lililoathiri usafirishaji wa nishati duniani na kuongeza bei ya mafuta.
BBC





