Mariah Carey avunja rekodi yake tena
Eric Buyanza
December 26, 2023
Share :
Kama kawaida yake kinapokuja kipindi hiki cha Krismasi...huwa ni muda wa maokoto kwa mwanamuziki mkongwe duniani mwanamama Mariah Carey (Queen of Christmass).
Namaanisha muda wa maokoto kwasababu ndio muda ambao ngoma zake za krismasi huchezwa au kupakuliwa zaidi kwenye mitandao mbalimbali ya muziki duniani.
Mariah amevunja tena rekodi ya muda wote kwenye 'Streams' za mtandao wa Spotify kwenye usiku wa mkesha wa Krismasi.
Wimbo wake "All I Want For Christmas Is You" ulitiririshwa mara 23,701,697 mwaka wa huu 2023 ukilinganisha na mwaka jana ambapo wimbo huo ulivunja rekodi pia kwa streams 21,273,357.